USHAURI NASAHA
Ushauri na sana
Ni mazungumzo kati ya mtu mwenye ujuzi,utaalam na uzoefu wa kusikiliza na kutoa mwongozo wa namna ya kutatua tatizo LA mtu au kikundi cha watu.
Ifahamike ushauri nasaha ni huduma inayohitaji watu wawili au zaidi yaani;
1:mnasihi(mshauri) huyu ni mmoja tu na si zaidi
2:mshauriwa au mteja wa mshauri (huwa mmoja au kundi)
Mshauri huhitaji mshauriwa ili kufanikisha zoezi zima LA ushauri na saha
Kwa nchi zilizoendelea kuna vitu vya ushauri na saha ambapo mshauri(therapist)huwa anasubiri mteja ili kufanikisha kazi ya utherapy au ushauri
Kwa nchi za ulimwengu wa tatu ni ngumu kuona Kitu km hicho unless otherwise hospital... Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi wa nchi hizo hawapendi kutembelea vituo vya afya mpaka wapatwe na magonjwa hivyo hivyo kwa vituo vya ushauri.Watu wengi ni wagonjwa bila kutambua na huhitaji kushauriwa ili kuenenda vizuri na jamii
Chunguza! Unakuta mtu ana bima ya afya mpaka mwaka unaisha hajawahi kwenda hospital kuchunguza afya pia hata apatwe na tatizo wengi hugugumia na wachache huwaeleza marafiki ambao huwakomboa kwa ushauri wao
MISINGI/SIFA ZA USHAURI NA UNASIHI
1 Lazima kuwe na usiri
Ni lazima kuwepo na usiri has a sana mnasihi ni lazima atunze siri ili kuboresha Uhuru wa mnasihiwa wa kujieleza.Pia mazungumzo ni lazima yawe ya siri hayatakiwi kusikika mahali pengine popote pale isipokuwa:
¹:kwa idhini/ridhaa ya mnasihiwa.Hapa ikiwa mnasihiwa amekubali na ameridhia tatizo lake lisemwe kwingine ndipo mnasihi unaruhusiwa kusema mambo hayo kwa mtu au watu mfano mteja(mshauriwa)anatatizo la kupata ujauzito ikiwa ni mwanafunzi au anatatizo la kubakwa mnasihi haruhusiwi kusema kwa mtu yeyote hata iwe ni wazazi wa binti isipokuwa kma yeye mnasihiwa akubali lifikishwe kwa wazazi
²:kwa matumizi ya kitabibu
Iwapo labda inahitajika kupima kuona km kweli mtu amepatwa na tatizo ni ruksa kutumika au kuomba kuthibitisha km kweli tatizo limetokea.mfano mtoto/mwanafunzi amebakwa hivyo anapokuja kwa mnasihii huweza kwenda kupima kujua madhara yaliyo mpata pia kutibu tatizo hivyo ni lazima kuwe na uwazi kwa daktari ili apate kulitibu na kulishughjlikia tatizo ipqsavyo.
³:kwa matumizi ya kisheria
Mnasihiwa na mnasihi huweza kukubaliana kwenda kwenye vyombo vya sheria pale tatizo lknapohitajika hivyo ni lazima kuwe na maelezo ya wazi kwenye vyombo hivyo ili kukomesha tatizo au hatua za kisheria kufuatwa ili kutuliza tatizo mfano mwanafunzi aliyepewa ujauzito wanaweza kukubaliana na mnasihi kutoa taarifa ikiwa ananyanyaswa au anakatazwa kusema pia km anaona hajatendewa hali kma kitu hicho ni lazima kitolewe taarifa pia ili mtuhumiwa apate kukamatwa na kufikishwa sehemu husika pia km imetokea mwizi labda anafahamika na mnasihiwa anaweza kutoa taarifa...
NB:Endapo mnasihi akatoa siri bila idhini au ridhaa ya mnasihiwa,mnasihiwa ana haki ya kumshitaki mtu huyu na hafai kuitwa mshauri
2.Kujiheshimu na kumheshimu mteja
Mnasihi anapaswa kuwa na ukadibu wa kiasi pia kumheshimu mnasihiwa ili kufanikisha zoezi la unasihi na kushauri usiwe mtu anatoka kisha anasema kwingine mfano yule mwanafunzi ni mwathirika,Pia kutomtongoza ikiwa mnasihiwa ni wa jinsia tofauti
3:Kuzungumza lugha fasaha
Mnasihi anapaswa kuzungumza lugha inayoeleweka na mteja wake ili kuleta maelewano na pia kuleta Uhuru kwa mnasihiwa wa kujieleza
4:Upole na uwazi
Mnasihi ni lazima awe mpole ili kuweza kumpa nafasi mteja wake kumpa nafasi ya kujieleza pia uwazi ni muhimu ili kuweza kufanya kazi ya unasihi iwe rahisi pia kumpa nafasi mteja kufungua hadi siri za moyoni
5:Uwezo wa kutambua tabia za mnasihiwa
Kurahisisha kazi ya unasihi mnasihi anatakiwa kufahamu tabia za wapi ili kupunguza na kuepuka matatizo yasiyo ya lazma mfano mnasihiwa mwenye tabia ya umalaya ni vyema kumtambua kabla ya kumnasihi ili kusaidia kutoleta tatizo jingine ni vyema km mada ya mapenzi chokochoko za tatizo lingine zinapotokea ni vyema kuahirisha kazi ya unasihi
6:Kuheshimu mila na desteri au tamaduni za jamii
Mila ma desturi pia tamaduni za mahali husika ni vyema kuzingatiwa mfano ikiwa si ruksa kumshika au kugusana ni vyema kufuata taratibu zote pia ikiwa ni lazima kukaa sehemu ya wazi ni vyema kufanya hivo kuepukana na matatizo yasiyo ya lazima mfano mnasihi anazungumzia ufugaji wa nguruwe na faida zake ni vyema kutafuta watu wanaotumia ila sio mtu anaenda Zanzibar anashauri mtu kutumia nguruwe hapo anaeza kufukuzwa au kutofanikiwa katika kazi yake pia ni lazima kutambua mila na desturi za sehemu husika
8:mahusiano kati ya mnasihiwa na mnasihi
Mahusiano mazuri husaidia sana katika unasihi ila tu yasizidi mipaka mpaka kwenye mapenzi pia ni vyema kukatisha kazi ikiwa kuna hadithi zinazoelekea kwenye kutengenezA tatizo jingine
VIKWAZO VYA UNASIHI
Ni hali inayofanya mahusiano kati ya mnasihi NA mteja wake yasiendelee
Vifuatavyo ni vikwazo vya unasihi;
a):muda
Tendo la kunasihi linahitani muda wa kutosha ambapo ni vigumu kupata muda wa kutosha hivyo linaweza kufanyika kwa muda mrefu hivyo kupelekea tatizo kujua
b):uwezo wa mnasihi
Mnasihi ni lazima awe na utaalamu na afahamu taratibu na kanuni za unasihi km ilivyoelekezwa hapo juu Anaweza kuwa amesoma au anaweza kuwa na uzoefu wa kutatua tatizo hilo
c):utawala wa mahali husika mfano shule au kijiji huenda kukapelekea kazi ya unasihi kuwa ngumu
Maoni
Chapisha Maoni