HKaswende ni ugonjwa unaoambukiza haraka sana,
mara nyingi kwa kufanya ngono. Ugonjwa huu
huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko
wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi,
au kwenye ngozi laini zenye majimaji za ukeni,
kwenye sehemu ya haja kutolea haja kubwa, na
midomo.
Kwa hiyo njia kuu ambayo husabaisha kuenea kwa
ugonjwa huu ni kupitia ngono ya kawaida, ya
kutumia midomo na ile ya kinyume na maumbile.
Mara chache ugonjwa huu huweza kuambukiza kwa
kubusiana au kugusana miili. Pamoja na kuwa
ugonjwa huambukiza kupitia michubuko, mara
nyingi michubuko hatarishi haitambulikani.
Mtu aliyeambukizwa huwa hajielewi na hivyo
kumwambukiza mpenzi wake.
Kaswende haiambukizi kwa kuchangia vyoo, vitasa
vya milango, mabwawa ya kuogelea, kuchangia
nguo au vyombo vya chakula.
Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye
Treponema pallidum, ambaye pia huitwa
spirochetes kutokana na umbo lake la mzunguko.
Viumbe hawa hujipenyeza kwenye ngozi laini
inayotanda midomo au sehemu nyeti.
Mwanamke mwenye mimba na ugonjwa huu
anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni
kupitia placenta au wakati wa kuzaliwa. Aina hii ya
kaswende huitwa congenital syphilis, na inaweza
kusababisha kujifungua mtoto mfu au mtoto akafa
muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Watoto wengi hawaonyeshi dalili wanapozaliwa.
Baadaye watoto huota vijipele, hupata matatizo ya
meno, na kubonyea kwa mfupa wa pua – hali
inayoitwa saddle nose, kuwa viziwi, kuwa na watoto
wa jicho na kifafa.
Ugonjwa wa kaswende hugawanywa katika hatua na
kila hatua ikiwa na dalili tofauti, lakini wakati
mwingine hakuna dalili zitakazojitokeza kwa miaka
mingi.
Uambukizaji unatokea kwenye hatua ya kwanza, ya
pili na mara chache mwanzoni mwa hatua ya latent
phase.
Hatua Ya kwanza Ya Kaswende – Primary Syphilis
Kaswende huanza kama mchubuko mmoja (au zaidi
ya mmoja) mgumu usio na maumivu unaojulikana
kama chancre kwenye sehemu za siri, kwenye
mdomo, au kwenye ngoz,i siku 10-90 (wastani wa
miezi 3) baada ya maambukizi.
Mchubuko huu unaweza kubaki hapo bila kuleta
usumbufu kwa kipindi kirefu na hata maiaka mingi.
Mchubuko huu wa mviringo hutokea kwenye eneo la
maambuikizi. Hata bila ya tiba yo yote, mchubuko
huu unaweza ukapona wenyewe bila kuacha kovu
katika wiki sita.
Hatua Ya Pili Ya Kaswende – Secondary Syphilis.
Hatua ya pili inaweza ikadumu kwa mwezi mmoja
hadi miezi sita ikianza kama wiki sita hadi miezi
sita baada ya maambukizi. Katika hatua ya pili,
vijipele huota mara nyingi vikianzia mgongoni na
kuenea mwili mzima, pamoja na kwenye viganja vya
mikono na kwenye nyayo. Vijipele hivi huwa vya
mviringo vyenye rangi nyekundu au vyenye wekundu
wa kahawia.
Michubuko inayofanana na chunjua hutokea kwenye
sehemu za midomo na mkundu. Vile kutatokea
maumivu ya misuli, homa, kukauka koo, kuvimba
tezi, kupunyuka nywele, kukonda na uchovu wa
mwili.
Latent Syphilis
Kama tiba ya kaswende ya hatua ya pili haitatolewa,
ugonjwa utaendelea kwenye hatua iitwayo latent
stage. Katika hatua hii inayoweza kudumu kwa
miaka kadhaa, mwili utautunza ugonjwa bila
kuonyesha dalili zo zote. Pamoja na kuwa hakuna
dalili zo zote zitakazoonekana, ugonjwa huu
unaweza kuendelea kwenye hatua ya mwisho.
Hatua Ya Tatu Ya Kaswende – Tertiary syphilis
Asilimia 15 ya watu ambao hawakupata tiba kwenye
hatua ya pili ya kaswende watapata kaswende ya
hatua ya tatu – tertiary syphilis. Hatua hii inatokea
miaka 10 hadi 30 baada ya dalili za mwanzo za
kaswende. Dalili za kaswende za hatua hii ni
pamoja na kushindwa kumudu matumizi ya viungo
vya mwili, ganzi, upofu, ugonjwa wa kupoteza
kumbukumbu, madhara kwenye moyo na mishipa ya
damu, madhara kwenye ini, mifupa na maungio ya
mifupa. Kifo huweza kutokea kutokana na uharibifu
wa viungo vya mwili.
Kuwahi kumpa tiba mgonjwa wa kaswende ni
muhimu kwani kuchelewa kunaweza kumletea
madhara makubwa ya mwili au kifo. Kama ugonjwa
haujazidi mwaka mmoja, mara nyngi dozi moja ya
ya penicillin hutosha. Kaswende iliyoendelea kwenye
hatua nyingine, dozi nyingine zitahitajika
Maoni
Chapisha Maoni