Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MALAIKA MIKAEL

MALAIKA MIKAEL NI NANI?

KULINGANA na Biblia, kuna mamilioni ya malaika
wanaoishi katika makao ya kiroho. ( Danieli 7:9, 10;
Ufunuo 5:11 ) Kutoka mwanzo hadi mwisho,
Maandiko mara nyingi hurejezea malaika walio
waaminifu kwa Mungu. Hata hivyo, ni wawili tu kati
ya viumbe hao wa kiroho wanaotajwa kwa majina.
Mmoja wao ni malaika Gabrieli, aliyewapelekea
watu watatu tofauti-tofauti ujumbe kutoka kwa
Mungu kwa kipindi cha miaka 600 hivi. (Danieli
9:20-22; Luka 1:8-19, 26-28 ) Malaika mwingine
anayetajwa kwa jina katika Biblia ni Mikaeli.
Bila shaka, Mikaeli ni malaika mwenye cheo cha
pekee. Kwa mfano, katika kitabu cha Danieli,
Mikaeli anatajwa kuwa anapigana na roho waovu
kwa niaba ya watu wa Yehova. (Danieli 10:13; 12:1 )
Katika barua iliyopuliziwa ya Yuda, Mikaeli
amshambulia Shetani katika bishano juu ya mwili wa
Musa. ( Yuda 9 ) Kitabu cha Ufunuo chaonyesha
kwamba Mikaeli alipigana na Shetani na malaika
zake na kuwavurumisha chini kutoka mbinguni.
(Ufunuo 12:7-9 ) Hakuna malaika mwingine yeyote
anayeonyeshwa kuwa mwenye uwezo na mwenye
mamlaka kubwa kama hiyo juu ya maadui wa
Mungu. Basi, si ajabu kwamba Biblia kwa kufaa
inamtaja Mikaeli kama “yule malaika mkuu.”
Ubishi Kuhusu Mikaeli
Dini za Jumuiya ya Wakristo na vilevile dini ya
Kiyahudi na ya Kiislamu, zina maoni
yanayotofautiana kuhusu malaika. Baadhi ya maoni
yao hayaeleweki. Kwa mfano, kamusi ya The Anchor
Bible Dictionary inaeleza: “Huenda kuna malaika
mmoja mkuu na/au kikundi kidogo cha malaika
wakuu (kwa kawaida wanne au saba).” Kulingana na
kamusi ya The Imperial Bible-Dictionary, Mikaeli ni
“jina la kiumbe mwenye uwezo unaozidi ule wa
wanadamu, ambaye watu wamekuwa na maoni
mawili yanayopingana kumhusu, eti huenda yeye ni
Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, au kwamba
yeye ndiye mmoja wa wale waitwao malaika wakuu
saba.”
Katika desturi za Kiyahudi, malaika hao wakuu saba
ni, Gabrieli, Yeremieli, Mikaeli, Ragueli, Rafaeli,
Sarieli, na Urieli. Kwa upande mwingine, Waislamu
wanaamini katika malaika wakuu wanne, Jibril,
Mikal, Izrail, na Israfil. Wakatoliki pia wanaamini
katika malaika wakuu wanne: Mikaeli, Gabrieli,
Rafaeli, na Urieli. Biblia inasema nini? Je, kuna
malaika wakuu wengi?
Jibu la Biblia
Katika Biblia, hakuna malaika mkuu mwingine
anayetajwa ila Mikaeli, wala Maandiko hayatumii
usemi “malaika mkuu” katika wingi. Biblia inamtaja
Mikaeli kuwa yule malaika mkuu, kuonyesha
kwamba ni yeye pekee aliye na cheo hicho. Kwa
hivyo, inafaa kusema kwamba Yehova Mungu
amempa mmoja tu wa viumbe wake wa mbinguni
mamlaka yote juu ya malaika wengine wote.
Mbali na Muumba pekee, Yesu Kristo ndiye mtu
mmoja tu mwaminifu anayetajwa kuwa na malaika
wanaojitiisha chini yake. ( Mathayo 13:41; 16:27;
24:31 ) Mtume Paulo alitaja wazi juu ya “Bwana
Yesu” na “malaika zake wenye
nguvu.” (2 Wathesalonike 1:7 ) Na Petro alisema
hivi kumhusu Yesu aliyefufuliwa: “Yeye yuko kwenye
mkono wa kuume wa Mungu, kwa maana alienda
akishika njia yake kuelekea mbinguni; na malaika na
mamlaka na nguvu vilifanywa kuwa vyenye kutiishwa
kwake.”— 1 Petro 3:22 .
Ijapokuwa hakuna taarifa katika Biblia
inayomtambulisha Yesu kwa wazi kuwa Mikaeli yule
malaika mkuu, kuna andiko moja ambalo
linamhusisha Yesu na cheo cha malaika mkuu.
Katika barua yake kwa Wathesalonike, mtume Paulo
alitabiri: “Bwana mwenyewe atashuka kutoka
mbinguni akiwa na mwito wa kuamuru, akiwa na
sauti ya malaika mkuu na kwa tarumbeta ya Mungu,
na wale walio wafu katika muungano na Kristo
watafufuliwa kwanza.” (1 Wathesalonike 4:16 )
Andiko hili linamtaja Yesu kama ambaye tayari
amechukua mamlaka yake akiwa Mfalme wa
Kimesiya wa Mungu. Hata hivyo, anazungumza kwa
“sauti ya malaika mkuu.” Kumbuka pia kwamba,
ana uwezo wa kufufua wafu.
Akiwa duniani kama mwanadamu, Yesu alifufua
watu kadhaa. Kwa kufanya hivyo, alitumia mwito wa
kuamuru. Kwa mfano, alipomfufua mwana wa mjane
mmoja wa jiji la Naini, alisema: “Mwanamume
kijana, nakuambia, Inuka!” ( Luka 7:14, 15 ) Baadaye,
kabla tu ya kumfufua rafiki yake Lazaro, Yesu
‘alipaaza kilio kwa sauti kubwa: “Lazaro, njoo huku
nje!”’( Yohana 11:43 ) Lakini katika pindi hizi, Yesu
alisema kwa sauti ya mwanadamu mkamilifu.
Baada ya Yesu kufufuliwa, alikwezwa kwenye “cheo
cha juu zaidi” mbinguni akiwa kiumbe wa roho.
(Wafilipi 2:9 ) Sasa ana sauti ya malaika mkuu kwani
yeye si mwanadamu tena. Hivyo, wakati tarumbeta
ya Mungu ilipowatolea mwito “wale walio wafu
katika muungano na Kristo” wafufuliwe kwenda
mbinguni, Yesu alitoa “mwito wa kuamuru,” lakini
wakati huo “akiwa na sauti ya malaika mkuu.”
Inafaa basi kufikia mkataa kwamba ni malaika mkuu
pekee anayeweza kutoa mwito “akiwa na sauti ya
malaika mkuu.”
Ni kweli kwamba kuna malaika wengine wenye vyeo
vya juu, kama maserafi na makerubi. (Mwanzo
3:24; Isaya 6:2 ) Hata hivyo, Maandiko humrejezea
Yesu Kristo aliyefufuliwa kuwa mkuu wa malaika

wote—Mikaeli yule malaika mkuu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USHAURI NA UNASIHI

              USHAURI NASAHA    Ushauri na sana Ni mazungumzo kati ya mtu mwenye ujuzi,utaalam na uzoefu wa kusikiliza na kutoa mwongozo wa namna ya kutatua tatizo LA mtu au kikundi cha watu. Ifahamike ushauri nasaha ni huduma inayohitaji watu wawili au zaidi yaani;  1:mnasihi(mshauri) huyu ni mmoja tu na si zaidi  2:mshauriwa au mteja wa mshauri (huwa mmoja au kundi) Mshauri huhitaji mshauriwa ili kufanikisha zoezi zima LA ushauri na saha Kwa nchi zilizoendelea kuna vitu vya ushauri na saha ambapo mshauri(therapist)huwa anasubiri mteja ili kufanikisha kazi ya utherapy au ushauri Kwa nchi za ulimwengu wa tatu ni ngumu kuona Kitu km hicho unless otherwise hospital... Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi wa nchi hizo hawapendi kutembelea vituo vya afya mpaka wapatwe na magonjwa hivyo hivyo kwa vituo vya ushauri.Watu wengi ni wagonjwa bila kutambua na huhitaji kushauriwa ili kuenenda vizuri na jamii Chunguza! Unaku...

JINSI YA KUMSHIKA MPENZI WAKO

    JINSI YA KUMSHIKA MKE AU MPENZI WAKO      Wengi hulizwa na wapenzi wao wa dhati pengine ni kwasababu hawajui wafanye nini!    Kuna mbinu za kumfanya mke au mume atulie na wewe. Mini mwanamke anataka? --->Anahitaji mwanaume anayempa furaha.Anaemfurahisha muda wote na kupenda -->Anahitaji mwanaume atakaye taniana naye.Tambua kwamba utani hunogesha zaidi mapenzi yenu sio kila wakati mwanaume upo serious laah unataka uitwe kinyago cha kutishia watoto? -->mwanaume atakayekuwa baba wa familia mwenye msimamo thabiti asiyeyumbayumba yaani Mara huku Mara kule na anayempenda -->Anahitaji mwanaume anayemridhisha katika tendon la ndoa .Hakika utapendwa japo tatizo kubwa kwa sasa ni Wanaume kutowaridhisha wake zAo nikuibie tu siri kidogo ;usiwe na papara muwapo kitandani tulia ikiwezekana cheza nae kwanza kabla ya tendon lenyewe na hapo utaona matokeo yake lazima tuu atakupenda tatizo LA wengi ni ikisha chanua anachojua ni kupiga mzimamzima ...

USHAURI WA NDOA NA MAPENZI

IMEANDALIWA NA *R.M - Professor of psychology Ohio state University-USA; katika kiingereza* IMETAFSIRIWA NA *MAISHA LASTON MWAIPAJA (AKABHOFU!!!!) BA.ED(horns) UDSM - TANZANIA ; katika kiswahili* *ZINGATIA*:- _TAFSIRI HII SIYO RASMI_ Anaanza kwa kusema......"Mwanaume anaweza kuchepuka na bado akawa na upendo wa dhati kwa mke wake lakini mwanamke hawezi kuchepuka na akaendelea kumpenda mume wake kwa dhati.Nasema hivi kwasababu mwanaume hafanyi tendo la ndoa kwa hisia, mwanamke hawezi kufanya tendo la ndoa bila hisia mguso.Ndiyo maana wanaume wanahitaji mahali pa kufanya tendo la ndoa ila wanawake wanahitaji sababu ya kufanya tendo la ndoa. Wanawake wengi wanaoenda mahakamani kudai talaka kwa waume zao ni wale wachepukaji,mwanamke asiyechepuka hawezi kwenda mahakamani kudai talaka isipokuwa kama mumewe atakuwa amezidisha unyanyasaji wa kimwili na kiakili kiwango cha kukaribia kumuua mkewe. Wanaume hawawezi kubadili tendo la ndoa na upendo.Mwanaume anaweza kufanya tendo la ...